Tuesday, November 25, 2014

HAPPY NEW WEEK!!

Friday, August 15, 2014

PENNY KUFUNGA NDOA SOON!! 

Mtangazaji  wa 93.7  E-FM  kupitia  kipindi  cha  Genge,  DVJ Penny  ambaye  wiki  kadhaa  zilizopita  picha  zake  zilisambaa  mtandaoni  zikimuonyesha  akiwa  amevishwa  pete   ya  uchumba  huku  mwanaume  aliyefanya  tukio  hilo  akiwa  ni  kitendawili, hatimaye  mwanadada  huyo  ameibuka  na  kumuweka  wazi  mpenzi  wake…..

Akiongea   rafiki  wa  karibu  wa  Penny  amesema  kuwa  jamaa  aliyemvalisha  pete  ni  kigogo  mwenye  pesa  chafu  anayemiliki  migodi  kadhaa  ya  madini  anayefahamika  kwa  Jina  la  Johnson  raia  wa  Angola….

Akiongea  kwa  kirefu  zaidi, msichana  huyo  alisema,” Watu  wanaumiza  vichwa  vyao  kufikiri  ni  nani  aliyechukua  maamuzi  magumu  ya  kumvisha  pete  Penniel, lakini  ukweli  ni  kwamba  huyo  jamaa  ni  mtu  mwenye  pesa  chafu  raia  wa  Angola,”

Rafiki  huyo  amesema  kuwa  kutokana  na  jeuri  ya  pesa  ya  kigogo  huyo, Penny  anatarajia  kufanyiwa  bonge  la  harusi  na  watafanya  kila  namna  ili  Diamond  awe  mtumbuizaji  katika  sherehe  hiyo….

“Huko  kwao  Johnson  anamiliki  migodi  zaidi  ya  kumi  ya  Almasi  na  yupo  hapa  nchini  kwa  ajili  ya  uwekezaji, anampenda  sana  Penny  na  ameahidi  kumfanyia  kila  atakacho,”  alisema  msichana  huyo.

Baada  ya  kupata  umbea  huo,  Mwandishi  alimtafuta  Penny  kupitia  simu  yake  ya  mkononi  na  kumhoji  juu  ya  taarifa  hizo  ambapo  alikiri  kuwa  na  mchumba  na  kusema  ndoa  iko  karibuni.
penny
“Nimeshakuwa  sasa, hivyo  nahitaji  kuolewa,  ni  kweli  nina  mchumba  na  ni  raia  wa  Angola, Inshaaalah  Mungu  akipenda  mambo  mazuri  yanakuja, ntakutaarifu,” alisema  Penny  lipoulizwa  kuhusu  Diamond  kutumbuiza  kwenye  harusi  yake, Penny  alijibu;
“Kutakuwa  na  wasanii  wengu  tu  sasa  na  yeye  kama  atapokea  mwaliko  wa  kuja  kutubuiza  atapatiwa  nafasi, akiona  vipi, halazimishwi.

Saturday, July 19, 2014

FAHAMU JINSI YA KUPATA MIMBA KWA KUTUMIA NGUVU ZA GIZA!!
Kabla  ya  ujio  wa  wakoloni, babu  zetu  walikuwa  wakiabudu  miungu  yao.Hakukuwa  na  dini  wala  tiba  za  kisasa.

Kwa  kuwa  IMANI  huponya, ni  ukweli  usiopingika  kwamba  maombi  yao  na  tiba  zao  za  asili  ziliwasaidia  sana katika  kutimiza  shughuli  zao  za  maisha  ya  kila  siku.

Yafuatayo  ni  mambo  machache  ambayo  yalikuwa  yakipatiwa  ufumbuzi  kwa  nguvu  za  giza.

1. Kupendwa  na  mpenzi  wako.
-Ili  upendwe  na  mpenzi  wako, unachotakiwa  kufanya  ni  kuweka  mbegu  kavu  za  nyanya  kwenye  kitambaa  kidogo  chekundu  au  rangi  ya  damu  ya  mzee  na  uwe  unaibeba  kila  siku  unapokutana  nae  au  unaweza  kuiweka  kwenye  pochi  yake  kila  unapokwenda  kwake.

2:Kujua  siri  zilizojificha  za  mpenzi  wako.
Kama   una  mpenzi  au  mtu  ambaye  anakuficha  jambo  na  unataka  kulijua,chukua  viazi  tisa,kata  katika  shepu  ya  pembe  tatu  kisha  weka  chini  ya  kitanda  chako  kwa  wiki  moja, siri  zake  utazigundua  ama  kwa  kuambiwa  na  kuoana  au  yeye  mwenyewe  atakwambia  bila  kujijua .

3.Kupata  ujauzito.
Ili  kupata  mbegu  zitakazo sababisha  mwanamke  upate  ujauzito,weka  vipande  vitatu  vya  mizizi  ya  mihogo  chini  ya  kitanda  kila  siku.

Kwa  upande  wa  mwanamke, ili  ufanikiwe  kumpa  ujauzito  mwanamke,kunywa  juisi  ya  karoti  kila  siku  huku  mawazo  yako  yote  yakifikilia  suala  hilo.

--Mandai, Uwazi 

Tuesday, June 10, 2014

HAYA NDIO YALIYOJIRI KWENYE UZINDUZI WA LIFT JIJINI MBEYA��

U.T.I

U.T.I kirefu chake ni Urinary Tract Infection ni maambukizi ya bakteria mbalimbali wanaoshambulia  mfumo wa mkojo, yaani kwenye figo (kidney), kibofu cha mkojo na mifereji inayotoa mkojo (urethra)
Mifereji inayotoa mkojo kwenye figo (ureter) na mfereji unaotoa mkojo nje, mara nyingi bakteria hushambulia sehemu za chini za mfumo wa mkojo yaani urinary bladder na kitaalamu kuitwa bladder infection.
Bakteria hao baada ya kumuingia binadamu hupona mara moja  pindi mgonjwa anapoanza dozi lakini kama wadudu hawa hawatatibiwa vizuri wanaweza kupanda na kushambulia figo na mshipa unaounga sehemu hiyo uitwao renal pelvis na kuleta madhara makubwa, hivyo kusababisha ugonjwa wa figo.
Kuna wadudu wanaotoka kwenye utumbo mkubwa wa binadamu ambao kila binadamu anaishi nao, hawa husaidia kulinda mwili na kitaalamu hujulikana kama  normal flora na huwa ni askari wa mwili.
Vijidudu hivyo hushuka hadi kwenye mlango wa  haja kubwa na kuenea mpaka sehemu za siri. Kama wataingia kwenye mfumo wa mkojo hushambulia sehemu hizo kwani wadudu  hao wanakuwa hawajazoea mazingira ya sehemu za mkojo.
WANAWAKE WANAVYOSHAMBULIWA NA UTI
Mara nyingi wanawake  ndiyo wanaoshambuliwa kirahisi na bakteria wa UTI  kutokana na maumbile yao ya sehemu za siri.
Sababu kubwa ya kushambuliwa kirahisi ni kwa kuwa wanakuwa na mfereji mfupi wa kutoa nje mkojo (shot urethra).
Sababu nyingine inayosababisha UTI ni kutokumywa maji kwa wingi, hivyo kushindwa kwenda haja ndogo mara kwa mara.
Kama mtu ana ugonjwa wa mawe kwenye figo (kidney stone) pia kwa wanaume  wenye ugonjwa wa kuvimba tezi la manii (enlarged prostate), wana uwezekano wa kukumbwa na maradhi haya.